JOBS AT KIGAMBONI DISTRICT




TANGAZO LA NAFASI YA KAZI 
 MWENYEKITI WA BODI YA AJIRA YA HALMASHAURI YA MANISPAA YA KIGAMBONI KWA KIPINDI CHA MWAKA 2017 HADI 2020


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni anawatangazia wananchi wote kuwa kuna nafasi wazi ya Mwenyekiti wa Bodi ya Ajira ya Manispaa kwa kipindi cha mwaka 2017/2018– 2019/2020.



SIFA ZA MWOMBAJI:
1.    Awe Raia wa Tanzania, Mkazi wa Manispaa ya Kigamboni mwenye umri kati ya miaka 45 – 65
2.    Awe mwadilifu
3.    Awe na Taaluma katika mojawapo ya fani zifuatazo:-
       Menejimenti ya Rasilimali watu (Human Resources Management).
       Utawala wa Umma (Public Administration)
       Sheria (Law).
4.    Awe na uzoefu mkubwa katika masuala ya Rasilimali watu, Utawala na Sheria katika Utumishi wa umma.
5.    Aidha kazi ya mwenyekiti wa bodi ya ajira haina mshahara bali mwenyekiti wa bodi ya ajira atalipwa posho za vikao vya bodi ya ajira kadiri vitakapajitokeza au kadiri atakavyohudhuria.
6.    Kipaumbele kitatolewa kwa wakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni


MAELEKEZO:
1.    Waombaji wote watume barua za maombi zikiwa na viambatisho vifuatavyo:-
    i)    Cheti cha kuzaliwa
    ii)    Vivuli vya vyeti vya masomo na Taaluma (Certified)
   iii)    Barua ya utambulisho toka kwa Mwenyekiti wa Serikali za Mitaa ikiwa na picha ndogo ya hivi karibuni.
   iv)    Wasifu binafsi (CV)
2.    Barua toka kwa wadhamini wawili (2) zikiwa na anuani kamili.
3.    Mwisho wa kutuma maombi ni tarehe 11.09.2017
4.    Barua zote za maombi zitumwe kwa anuani ifuatayo:-


Mkurugenzi wa Manispaa,
Manispaa ya Kigamboni,
S.L.P 36009,
KIGAMBONI, DAR ES SALAAM.


Imetolewa na:
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA KIGAMBONI.

Comments