“Anthony Ralston” kutoka kuokota mipira hadi kuvimbiana na mchezaji ghali wa dunia, mashabiki wa Celtic wamuita Shujaa

Celtic wamepigwa 5 kwa 0 nyumbani kwao na Barcelona, sio tukio zuri na ni aibu lakini mashabiki wa klabu hiyo wana kitu cha kuongea na kujisifu baada ya mchezo huo, ni jina la Anthony Ralston.
Huyu dogo alizaliwa mwaka 1998 mwishoni na hadi sasa ana miaka 18 tu, Ralston sio mchezaji tu wa Celtic bali ni muumini na mfuasi wa Celtic, maisha yake ya utoto ni Celtic, amekulia Celtic na humuambii kitu kuhusu Celtic.
Anthony Ralston alikuwa muokota mipira “ball boy” wa klabu ya Celtic kazi ambayo baadae ilimfanya aamini siku moja atakuwa moha kati ya mashujaa wa Celtic na usiku wa jana pamoha na kipigo lakini mashabiki wa Celtic wamemchukulia Ralston kama shujaa wao.
“Nilikuwa naokota mipira hiyo ndio ilikuwa kazi yangu, wakati Celtic tunashinda bao 2 dhidi ya Barcelona nilikuwepo na kuanzia hapo nikaamini kuwa naweza kupambana na mimi nikaichezea Celtic” alisema Ralston.
“Kuwa uwanjani kuitumikia Celtic hiyo ndiyo ilikuwa ndoto yangu ya muda mrefu, kocha aliniambia wiki moja kabla kwamba nitacheza na ilinipa muda kujiandaa kwa ajili ya mchezo huu”
Unaweza kupata picha mchezaji kinda kama huyu Ralston leo mara paap anakutana na Neymar Dos Santos mchezaji ambaye dunia inamzungumzia sana kwa sasa, huku dau la £198m la kwenda PSG likimfanya atishe zaidi.
Lakini Ralston bila uoga alikuwa akila bega kwa bega na Neymar bila uoga, japokuwa walishindwa kuizima PSG lakini Ralston alikuwa suprise package katika kikosi cha Celtic kiasi cha kumfanya Neymar  kupanick baada ya mchezo.
Mpira ukaisha, wakati umeisha Ralston aliamua kumfuata mchezaji ghali wa dunia Neymar na kumpa mkono lakini Neymar alikataa mkono wa beki huyu, beki huyu bila uoga badala ya kuogopa alimcheka Neymar kitu ambacho kilimkera sana Mbrazil huyu.
“Nilipoambiwa nitacheza nilijua nitakutana na Neymar, sikumuogopa na nilikuwa tayari kupambana, nilimuona kama mchezaji mwingine tu na nilijiandaa kucheza kama mechi ya kawaida” alianza Ralston kumzungunzia Neymar.
“Kilichotokea kama aliamua kiwe vile acha kiwe hivyo ila mimi sijali na sidhani kama Neymar anaweza kunikosesha usingizi hata mara moja”  alisema Ralston ambaye tangu azaliwe yeye amekuwa akiitumikia tu Celtic japo mwaka jana alipelekwa QPR kwa mkopo.

Comments